Mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya wamekubaliana kulitangaza jeshi la Walinzi wa Mapinduzi la Iran (IRGC) kuwa ni kundi la kigaidi. Akizungumza mjini Brussels wakati wa mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa EU, Mkuu wa sera za kigeni wa umoja huo Kaja Kallas amesema “utawala wowote unaowaua maelfu ya watu wake unajiangamiza wenyewe.”
Msimamo huo wa pamoja unaanzisha utaratibu wa kisheria wa kurasimisha tamko hilo ambalo linachukuliwa kuwa la ishara kubwa kwa sababu jeshi hilo tayari limewekewa vikwazo na EU kwa ukiukaji wa haki za binadamu.
Huku baadhi ya mawaziri wa EU wakidokeza kwamba hadi watu 30,000 huenda waliuawa katika ukandamizaji mkali dhidi ya maandamano ambayo yameikumba Iran, shinikizo limeongezeka kwa Umoja wa Ulaya kuchukua uamuzi huo.
Chanzo; Dw