Jeshi la Uganda limekiri kuwakamata kwa muda mfupi Barbara “Barbie” Kyagulanyi, mke wa kiongozi wa upinzani Robert Kyagulanyi maarufu Bobi Wine, kabla ya kumuachilia huru, likisema alisaidia katika jitihada za kumtafuta mumewe.
Kupitia mtandao wa X, Kiongozi wa Jeshi la Ulinzi wa Wananchi wa Uganda, Jenerali Muhoozi Kainerugaba, alithibitisha tukio hilo lililotokea usiku wa Januari 23 katika eneo la Magere, Wilaya ya Wakiso, na kukanusha madai ya kudhalilishwa kwa Barbie.
Alisisitiza kuwa lengo la jeshi ni kumtafuta Bobi Wine, ambaye yuko mafichoni kufuatia uchaguzi wa urais wa Januari 15 uliompa ushindi Rais Yoweri Museveni kwa muhula wa saba.
Chanzo; Nipashe