Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Video ya Sokwe ya Obama, Trump Agoma Kuomba Radhi Adai Hana Kosa

Rais wa Marekani Donald Trump amefuta video aliyopakia kwenye Truth Social baada ya kukosolewa vikali na viongozi wa Republican na Democrat.

Video hiyo ya takriban dakika moja ilidai kuwepo kwa udanganyifu kwenye uchaguzi wa 2020, kisha mwishoni ikaonyesha sura za Barack na Michelle Obama zikipachikwa juu ya miili ya sokwe huku wimbo The Lion Sleeps Tonight ukichezwa.

Ikulu ya Marekani ilisema video hiyo ilipakiwa kimakosa, huku Trump akikataa kuomba radhi akisisitiza kuwa “hakufanya kosa.” Wakosoaji waliita tukio hilo la kukera na lenye mwelekeo wa ubaguzi wa rangi.

 

 

Chanzo; Dw

Kuhusiana na mada hii: