Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Wafungwa 200 Wagoma Kula Wadai Hawatafaidika na Sheria

Zaidi ya wafungwa 200 wa kisiasa wa Venezuela waliingia kwenye mgomo wa kula siku ya Jumapili kama ishara ya kushinikisha waachiliwe huru chini ya sheria mpya ya msamaha ambayo haijumuishi wengi wao.

Wafungwa katika gereza la Rodeo I, takriban kilomita 40 (maili 25) mashariki mwa mji mkuu Caracas, walipiga kelele kwa wapendwa wao kama sehemu ya maandamano hayo.

Mgomo wa kula ulioanza Ijumaa usiku, ulikuja baada ya wafungwa kulalamika kuwa hawatafaidika na sheria hiyo kwa sababu haijumuishi kesi zinazohusisha wanajeshi, ambazo ndizo zinazozoeleka zaidi katika kituo hicho.

Hata hivyo kwa mujibuwa ndugu wa wafungwa hao, inasemekana sio wafungwa wote katika gereza hilo, walikuwa wakijiunga na mgomo wa kula.

 

 

Chanzo; Itv

Kuhusiana na mada hii: