Waendesha mashtaka nchini Kenya wamesema wataongeza watamfungilia mashtaka mengine ya mauaji Paul Mackenzie, mtu aliyejinadi kuwa mhubiri wa Kanisa la Good News International anayehusishwa na vifo vya mamia ya wafuasi wake alowaamuru kufunga kula na kunywa ili waende mbinguni.
Mkasa huo unaofahamika na wengi kama mauaji ya msitu wa Shakahola ulishuhudia miili ya zaidi ya watu 400 ikifukuliwa kwenye msitu mashariki mwa Kenya baada ya kufichuka kwa kanisa la siri lililodaiwa kuwa lilikuwa likiongozwa na Mackenzie.
Maafisa hao wa Kenya wamesema wataongeza mashtaka ya mauaji ya watu wengine 52 katika kijiji cha Binzaro.
Uchunguzi unaonyesha kanisa lake liliendelea na oparesheni hatarishi hata baada ya Shakahola kugunduliwa na Mackenzie kukamatwa.
Awali, inadaiwa aliwashawishi wafuasi kujinyima chakula ili “kuonana na Yesu” na kuhakikisha hakuna aliyetoka msituni salama.
Tukio hili lililoibua mshangao linazingatiwa kuwa mojawapo ya mauaji mabaya zaidi yanayohusiana na madhehebu ya dini duniani.
Chanzo; Dw