Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Majaliwa Alivyoingia Kibabe Belarus

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Julai 21, 2025 amewasili nchini Belarus kuanza ziara ya kikazi nchini humo. Kwenye Uwanja wa Ndege wa Kinsk alipokelewa na Naibu Waziri Mkuu wa Beralus, Viktor Karankevich. 

Katika ziara hiyo siku ya Kwanza Mheshimiwa Waziri Mkuu ataweka shada la maua katika mnara wa mashujaa wa Jamhuri ya Beralus.

 Pia atatembelea kiwanda cha kutengeneza Matrekta na vifaa mbalimbali vya kilimo (Minsk Tractor Plant) na baadae atakutana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Belarus Mhe. Alexander Turchin.



Katika ziara hiyo ameambatana na Balozi wa Tanzania Urusi na Belarusi, Frederick Ibrahim Kibuta , Waziri wa Nchi, Afisi ya Rais, Kazi , Uchumi na Uwekezaji Zanzibar, Shariff Ali Shariff na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Cosato Chumi.

Kuhusiana na mada hii: