Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Hapi Ampa Faraja Ummy , Awatupia Jiwe Wachochezi

Katibu Mkuu wa Umoja wa Wazazi CCM Taifa, Ally Hapi amemuomba aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Tanga na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu pamoja na Wagombea wengine walioshindwa kwenye uchaguzi kuepuka Wapambe ambao wanaweza kupeleka uchonganishi baina ya Viongozi na Chama.

 

Hapi ameyasema hayo katika kikao kazi cha Kampeni za uchaguzi Jijini Tanga ambapo amekutana na makundi mbalimbali wakiwemo Wajasiriamali, Maafisa usafirishaji na Makundi maalumu ambapo wakati akiongea ametumia maandiko matakatifu ya Quran kuwafariji wote walioshindwa kwenye uchaguzi wa ndani wa Chama hicho na kuwaomba kuacha makundi na badala yake waungane kutafuta kura za CCM.

 

“Nasema haya sio kwasababu ya Ummy, kwasababu ya Wapambe, Wapambe msilie kuliko mwenye msiba haya yalishaandikwa kwenye kitabu kabla ya kuumbwa sisi tunakamilisha ratiba tu na mwenyenzi Mungu yupo pamoja na wenye kusubiri tuwaombee nchi hii kubwa sana” - Ally Hapi

 

Chanzo: Millard Ayo

Kuhusiana na mada hii: