Mgombea Urais kupitia chama tawala nchini Tanzania CCM Samia Suluhu Hassan amesema taifa hilo la Afrika mashariki linayo akiba ya kutoisha ya chakula kwa miezi iliyo salia kwa mwaka 2025.
“Akiba yetu ya Chakula sasa ni zaidi ya miezi minne mwaka mzima hatuwezi kufa njaa, tuna chakula cha kutosha lakini pia tunazalisha chakula kwa biashara” - Dkt. Samia
Ameyasema hayo kwenye kampeni za chama hicho mkoani Arusha Kaskazini mwa Tanzania na kuongeza kuwa, kwa sasa taiafa hilo linajipanga kuboresha kilimo cha biashara kinachojikita kidigitali ili kuendana na matakwa ya duania ya sasa.
Chanzo: Dw