Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, chama tawala, Stephen Wasira amesema kunung'unika na kufikisha ujumbe wa changamoto mbalimbali kwa njia ya maandamano kumepitwa na wakati kwa kusema Watanzania wanataka maendeleo ukiwemo ujenzi wa miundombinu muhimu ambayo itarahisisha shughuli za kiuchumi na ajira kwa wananchi.
Kiongozi huyo wa CCM ametoa matamshi hayo jana Septemba 28, 2025 wakati alipokuwa akizungumza na viongozi na wanachama wa chama chake wa majimbo ya Vunjo na Moshi Vijijini, mjini Moshi ikiwa sehemu ya kampeni ya chama hicho kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29 wa Tanzania. Tujadili wazo la mbinu mbadala la kufikisha hisia za umma kwa mamlaka.
Chanzo: Dw