Kamati Kuu ya Halmashauri kuu ya chama tawala nchini Tanzania CCM imelaani vitendo ilivyovitaja kuwa vya kihuni na uvunjifu wa amani vilivyofanywa na baadhi ya watu vilivyosababisha vifo na uharibifu wa mali za umma na za wananchi.
Hata hivyo taarifa ya kamati hiyo haikugusia madai ya mauaji yaliyofanyika wakati wa maandamano ya uchaguzi na kutajwa na mashirika tofauti yakiwemo ya utetezi wa haki za binadamu na chama cha upinzani Tanzania CHADEMA.
Aidha pia kamati hiyo iliyokutana leo mjini Dodoma katika kikao maalum cha kutafakari hali ya kisiasa baada ya uchaguzi wa Oktoba 29, imewapongeza wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura katika uchaguzi.
Chanzo; Dw