Wakati zikisalia wiki tatu kabla ya uchaguzi mkuu visiwani Zanzibar, mgombea urais anayetetea kiti chake, Hussein Ali Mwinyi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), na mpinzani wake mkuu ambaye pia ni makamu wake wa kwanza, Othman Masoud Othman wa chama cha ACT-Wazalendo, wanatupiana lawama juu ya uwezekano wa kuharibika kwa hali ya usalama katika visiwa hivyo ambavyo vimezowea kushuhudia matukio ya mauaji na uvunjwaji mkubwa wa haki za binaadamu kwenye historia ya miongo mitatu ya chaguzi za vyama vingi.
Chanzo: Dw