Msaniii wa filamu na Mwenyekiti wa Mama Ongea na Mwanao Steve Nyerere ametoa tathimini yake ya hali ya kisiasa ikiwa ni siku 24 toka kipenga cha kampeni za uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani uanze August 28, 2025.
Katika tathimini yake amedai vyama vingi vya upinzani havijaonyesha umwamba wao, tofuati na CCM ambao wameonekana kukubalika katika maeneo mengi kutokana na mikutano yao kuvutia maelfu ya watu.
Kwa upande mwingine akosoa vikali taarifa mbalimbali ambazo amekuwa akizitoa aliyekuwa Balozi wa Cuba na kada wa CCM kuhusu serikali yake ambayo ameitumia kwa miaka mingi.
Steve amedai Polepole kwa sasa ni kama mchekeshaji kwani toka aanze kutoa matamko yake amekuwa akipuuzwa hali ambayo umemuondolea mvuto wake.
Chanzo: Bongo 5