Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mtama Mkoani Lindi Nape Moses Nnauye amesema kuwa wanaohoji imani na dhamira ya Mgombea Urais wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kusimamia utu wa Watanzania ni Watu walioamua kujitoa akili, wakidhamiria kuwavuruga na kuwadanganya Watanzania wapenda utu na maendeleo ya Nchi yao Tanzania kuelekea uchaguzi mkuu.
Nnauye amebainisha hayo leo Jumatano Septemba 24, 2025 kwenye Viwanja vya Mtama wakati wa mkutano wa kampeni za Dkt. Samia, akibainisha kuwa tangu kuingia madarakani kwa Rais Samia, matendo, maelekeo na maneno yake mengi yamekuwa yakionesha dhamira yake njema katika kukuza, kustawisha na kuheshimisha utu wa Mtanzania kupitia huduma muhimu za kijamii pamoja na ustawi wa kiuchumi na kijamii.
Chanzo Millard Ayo