Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Mgombea Urais Akimbia Mkutano Kisa Wanachama Wachache

Baada ya wananchi mjini Sumbawanga mkoani Rukwa, wamesikitishwa na kitendo cha mgombea wa nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia Chama cha NCCR Mageuzi, Haji Ambari Khamisi kukacha kuwahutubia.

Wakizungumza baada ya kumalizika kwa mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Sabato mjini hapo, wamedai kwamba kitendo cha mgombea huyo kutohutubia kwa madai ya kukosa idadi kubwa ya watu si haki kwao.

Mchambuzi wa masuala ya kisiasa ambaye ni mkazi wa kitongoji cha Jangwani, Baraka Mwaisabila amesema pamoja na kuwepo kwa idadi ndogo ya watu lakini mgombe huyo alipaswa kuwahutubia wale waliojitokeza pasipo kusubiri hadi namba ya watu iwe kubwa kama ilivyo kwenye mikutano ya vyama vingine vya siasa.

"Sisi tumeacha kazi zetu tumakuja kusikiliza sera za mgombea huyo lakini sasa kitendo cha kufika uwanjani na kuondoka bila kuhutubia na kuwaacha viongozi mkoa, wilaya na wagombea wa udiwani wakifanya hivyo peke yao si sahihi,” amesema Mwaisabila.

Naye, Vicent Kuligi ambaye ni katibu wa Muungano wa taasisi zisizo za kiserikali mjini Sumbawanga, amesema mgombea huyo wa urais kufika eneo husika na kutozungumza na wananchi aliowakuta anaonyesha jinsi chama chake kinavyotumia vibaya rasilimali zake.

Chanzo: Nipashe

Kuhusiana na mada hii: