Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimekanusha madai ya Padri wa Kanisa Katoliki Dk Charles Kitima kuhusishwa na siasa za chama hicho kikieleza kwamba si mwanachama wa chama hicho na wala hajawahi kualikwa kufanya siasa za chama hicho.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka katika chama hicho, Padri Kitima hana kadi ya chama hicho na hajawahi kualikwa katika vikao rasmi vya chama hicho wala kufanya kampeni yoyote inayokihusisha chama hicho kama ambavyo imekuwa ikidaiwa na baadhi ya wananchi.
Katika barua iliyoandikwa na baadhi ya waumini wa Kanisa Katoliki Tanzania kwenda ubalozi wa kanisa hilo hapa nchini imedaiwa Padri Charles Kitima amekuwa akijihusisha na siasa za CHADEMA jambo ambalo ni kinyume na taratibu za kanisa hilo.
Waumini hao wameomba kuchukuliwa hatua dhidi ya Padri Kitima kwa kile kilichodaiwa kuharibu taswira ya kanisa hilo kwa kuonekana kujihusisha na harakati za kisiasa.
Chanzo; Nipashe