Mitandao ya video za kikubwa Pornhub, Redtube na YouPorn imesitishwa nchini Ufaransa ikiwa ni hatua ya kupinga sheria inayotaka mitandao hiyo kuanzisha mfumo wa kuhakiki umri wa watumiaji wake.
Hatua hiyo inakuja ikikiwa ni baada ya serikali ya Ufaransa kuanzisha sheria yenye lengo la kuwalinda watoto dhidi ya maudhui ya ngono ambapo sheria hiyo itaanza kufanya kazi June 7.
Waziri wa Mambo Kidigitali nchini Ufaransa, Clara Chappaz ameishutumu mitandao hiyo kwa kutotaka kutii sheria na kuwalinda watoto.
“Tunataka kufanya kazi na watengenezaji wa mifumo kuhakikisha kwamba watu wazima tu ndio wanaweza kuona maudhui ya kikubwa” amesema Chappaz.
Mitandao hiyo haijasema haitapatikana Ufaransa kwa muda gani, hata hivyo imesema inafanya mawasiliano ya ukaribu na mamlaka za nchi hiyo ili kurejea hewani.
Mitandao ya Ngono Yazimwa Ufaransa
