Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Chadema Kuomboleza kwa Siku Saba

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema kutokana na matukio ya kusikitisha yaliyosababisha vifo, majeruhi na kupotea kwa baadhi ya Wananchi wakati wa maandamano ya October 29, Chama hicho kinatangaza rasmi siku saba za maombolezo ya kitaifa kuanzia November 05 hadi November 11, 2025.

Akitangaza uamuzi huo leo November 04,2025, Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa CHADEMA Taifa, Brenda Rupia amesema ili kuonesha heshima kwa waliopoteza maisha katika maandamano hayo, bendera zote za CHADEMA katika ofisi za Chama zitapepea nusu mlingoti kila siku kuanzia saa 12:00 asubuhi hadi saa 12:00 jioni katika siku zote saba za maombolezo.

Bado Mamlaka za Serikali hazijataja idadi kamili ya Watu waliopoteza maisha katika maandamano hayo, tunaendelea kufuatilia.

 

Chanzo; Millard Ayo

Kuhusiana na mada hii: