Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu Dodoma chini ya Jaji Wilbert Chuma imetoa uamuzi wa maombi ya kibali cha kuwasilisha maombi ya mapitio ya Mahakama nambari 23617 lililowasilishwa na Luhaga Mpina dhidi ya Msajili wa Vyama vya Siasa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Chama cha ACT-Wazalendo, Jaji Chuma alikubaliana na maombi hayo kwa hoja kwamba maombi hayo yamekizi vigezo vyote vinavyotakiwa vya kuiridhisha Mahakama kutoa kibali cha kuwasilisha maombi ya mapitio.
“Kwa hatua hii sasa, Chama cha ACT-Wazalendo na ndugu Luhaga Mpina kitawasilisha rasmi maombi ya kufutwa kwa maamuzi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ndani ya siku 14 kama ilivyoelekezwa na Mahakama kupitia maamuzi ya Jaji Chuma”-imesema sehemu ya barua ya chama hicho.
Chanzo: Nipashe