Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Lissu Maswali Mazito Mahakamani, Ahoji Ratiba

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, amehoji ratiba ya Mahakama Kuu, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, baada ya kuonesha tarehe ya hukumu ya kesi ya uhaini inayomkabili, ilhali hadi sasa hakuna shahidi hata mmoja aliyesikilizwa.

Lissu aliwasilisha hoja tatu mbele ya jopo la majaji watatu likiongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru, likisaidiwa na Majaji James Karayemaha na Ferdinand Kiwonde, akisema anahitaji ufafanuzi wa masuala hayo kabla ya usikilizwaji wa kesi kuendelea.

“Nipo tayari, lakini kabla hatujaanza nina mambo matatu ambayo naomba Mahakama inipatie maelezo. Septemba 30, 2025, Naibu Msajili Livin Lyakinana aliniandikia barua kupitia kwa Mkuu wa Gereza la Ukonga, ambayo niliipokea Oktoba 2, 2025,” amesema Lissu.

Ameeleza kuwa barua hiyo ilielekeza awasilishe orodha ya watu 100 anaowataka wahudhurie kesi hiyo, wakiwemo mawakili, viongozi wa chama, wanachama na ndugu zake, na kwamba majibu yake yafikishwe kwa Naibu Msajili kabla ya saa 12 jioni ya Oktoba 3, 2025.

“Kwa kuwa nipo gerezani, sina mawasiliano na ndugu, mawakili wala viongozi, lakini nilijitahidi mwenyewe kuandaa orodha hiyo ndani ya muda,” amesema Lissu, akidai kuwa baadhi ya watu aliowataja walizuiwa kuingia mahakamani, akiwemo ndugu yake aliyesafiri kutoka Ujerumani.

“Leo nimeona ndugu yangu mwenyewe akizuiwa langoni. Kama mna orodha yangu, yeye ni namba 12. Amekuja kuona jinsi Mahakama za Tanzania zinavyotenda haki katika kesi hii ya uhaini,” amesema Lissu, akidai kuwa watu wengine pia walipigwa nje ya geti.

Amehoji: “Nataka kujua, hii ni Mahakama ya Polisi au Mahakama ya Tanzania? Nani anaamua nani aingie, Majaji, Polisi au wale wanaonishtaki kwa uhaini?

 

Chanzo: Nipashe

Kuhusiana na mada hii: