Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Nitajenga Barabara ya Mzunguko, Ahadi ya Samia Tabora

Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Dkt Samia Suluhu Hassan, amewaambia wananchi wa Tabora kuwa atajenga barabara ya mzunguko yenye urefu wa kilomita 82 ili kupunguza msongamano mkoani humo.

 

Ameeleza hayo, leo Ijumaa Septemba 12,2025 wakati akihitimisha kampeni zake za mkoa wa Tabora kabla ya kuelekea mkoani Kigoma kuendelea kusaka kura kupitia mikutano ya hadhara iliyoandaliwa na CCM.

 

Huku akishangiliwa na maelfu ya wananchi wa Tabora, Dkt Samia,amesema awamu ya pili, endapo atapata ridhaa Serikali atakayoingoza itajenga barabara ya mzunguko ili kupunguza msongamano ndani ya manispaa ya Tabora.

 

“Ninayo furaha kuwaeleza kuwa tunakuja na ujenzi wa barabara mpya ya mzunguko ya Tabora Mji. Tumeshafanya tathimini ya barabara hii itakayokuwa na urefu wa kilomita 82”

 

“Hii itahakikisha magari yote yasiyokuwa na ulazima wa kupita ndani ya mji wa Tabora, yanapita barabara ya nje kwenda yanakoelekea.Tunataka Tabora yenye historia kubwa, iwe na hadhi kubwa pia,”amesema Dkt Samia. Wakati huo huo Zuberi Ngomano mmoja ya Viongozi wa Maafisa Usafirishaji (Bodaboda) Mkoani Tabora chini ya uongozi wake kundi hilo limepata manufaa mengi ambayo yamechagiza maendeleo yao.

 

Chanzo: Clouds Tv

Kuhusiana na mada hii: