Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM CPA. Amos Makalla amesema Julai 26, 2025 chama hicho kitakuwa na Mkutano mkuu maalumu kwa njia ya mtandao ambao utatanguliwa na vikao vya Halmashauri na Kamati Kuu ya Chama.
Makalla amesema hayo jijini Dodoma leo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya chama hicho na kusema kuwa sababu mojawapo za kufanya mkutano huo ni pamoja na marekebisho madogo ya katiba ya chama hicho.
"Agenda ya mkutano mkuu huo ni marekebisho madogo ya katiba ya Chama cha mapinduzi kwahiyo asubuhi tutakuwa na kikao cha kamati kuu, halmashauri kuu na baadae mkutano mkuu na naomba niwathibitishie maandalizi ya mkutano huu yamekamilika katika Wilaya zetu na katika Mikoa yote"