Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Ahadi 11 za Dkt. Samia Ruvuma, Lindi na Mtwara

Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amehitimisha ziara yake ya kampeni katika mikoa ya Kusini—Ruvuma, Lindi na Mtwara kwa kutoa ahadi kadhaa zenye mwelekeo wa maendeleo makubwa.

Hapa chini nakuwekea baadhi ya mambo aliyoyaahidi wananchi wa ukanda huu:

1. RELI YA MTWARA - MBAMBA BAY
Dkt. Samia ameahidi kujenga reli ya kisasa itakayounganisha Mtwara na Mbamba Bay, ili kurahisisha usafirishaji wa mazao na bidhaa, na kuongeza kasi ya biashara Kusini.

2. CHUO CHA UHASIBU SONGEA.
Atajenga Chuo Kikuu cha Uhasibu Songea kitakachochukua wanafunzi zaidi ya 10,000, jambo litakalowezesha vijana wa Kusini kupata elimu ya juu bila kusafiri mbali.

3. RUVUMA KUWA UKANDA MAALUM WA KIBIASHARA.
Mkoa wa Ruvuma utawekewa sera maalum za uwekezaji na biashara, ili kuvutia wawekezaji na kuongeza fursa za ajira kwa wakazi wake.

4. BYPASS YA SONGEA
Kupunguza msongamano katikati ya Songea, Dkt. Samia ameahidi kujenga barabara ya kuzunguka mji, jambo litakalorahisisha usafiri na kupunguza foleni.

5. KITUO CHA KUDHIBITI WANYAMA WAHARIBIFU NAKAPANYA.
Ili kulinda kilimo, atajenga kituo maalum cha kudhibiti wanyama waharibifu wanaoathiri mashamba ya wakulima.

6. DRONES ZA WANYAMA
Serikali itanunua drones za kufukuza wanyama waharibifu na kusaidia katika kulinda mashamba ya wakulima wadogo na wakubwa.

7. MRADI WA GRIDI IMARA YA UMEME.
Dkt. Samia ameahidi kujenga mradi wa gridi imara ya umeme kutoka Songea–Tunduru–Masasi, ili kusogeza huduma ya umeme wa uhakika kwa wananchi na viwanda.

8. TAWI LA CHUO KIKUU DSM - RUANGWA
Dkt Samia ameahidi ujenzi wa tawi la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam huko Ruangwa, linalotarajiwa kuongeza fursa za elimu ya juu kwa vijana wa Kusini.

9. RUZUKU YA GESI.
Kupitia ruzuku ya gesi, akinamama wataweza kupata nishati safi na nafuu, kupunguza utegemezi wa kuni na mkaa.

10. KIWANJA CHA NDEGE LINDI.
Kiwanja cha Ndege Lindi
Ukarabati na ufufuaji wa kiwanja cha ndege cha Lindi utawezesha mkoa huo kufunguka zaidi kibiashara na kitalii.

11. TEKNOLOJIA ZA KISASA MASHAMBANI.
Dkt. Samia ameahidi kupeleka “akili unde mashambani”—yaani mbinu na teknolojia mpyakwa wakulima ili kuongeza tija na thamani.

 

Chanzo: Clouds Media

Kuhusiana na mada hii: