Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, John Heche amesema Chama hicho kinapinga vitendo vyovyote vya utekaji Nchini na kinazitaka Mamlaka kutumia njia sahihi katika kukamata Watu pale ambapo wanatuhumiwa kwa makosa mbalimbali.
Heche ametoa kauli hii leo nje ya viunga vya Mahakama Kuu ya Tanzania, Masijala Ndogo ya Dar es salaam baada ya kuahirishwa kwa kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama hicho Tundu Lissu.
Heche amesema Chama hicho kinataka kiambiwe wako wapi Watu waliochukuliwa “Sisi kama CHADEMA hatukubaliani na Mtu yeyote kutekwa kwenye Nchi hii kama Mtu ana kosa akamatwe Ndugu zake waarifiwe yuko wapi waende wakamuone, leo tunazungumza karibu siku ya sita Kiongozi wetu Ernest Mgawe Mwenyekiti wetu yuko ndani haruhusiwi kuonwa, huyu Mtu anazuiliwaje kuonwa, ameua ? amefanya nini hicho cha kumzuia kuonwa?” - John Heche.
Chanzo: Millard Ayo