Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Mpina Atamani Kufunguliwa Agombee Urais

Baada ya kesi aliyoifungua aliyekuwa mgombea wa kiti cha Urais wa Chama cha ACT Wazalendo Luhaga pamoja Chama chake cha ACT Wazalendo kupinga kuenguliwa kugombea nafasi hiyo katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 29 mwaka huu, hukumu kesi hiyo dhidi ya Serikali itatolewa Ijumaa Oktoba 10, 2025.

Akizungumza mara baada ya kusikilizwa kwa kesi hiyo, Luhaga Mpina amesema matamanio yake makuu ni kuona anaruhusiwa kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kuonesha utofauti wa kampeni baina ya vyama vingine na kutimiza kusudio lake la kuongoza nchi baada ya kushinda uchaguzi, akibainisha kuwa Taifa linahitaji viongozi wa aina yake.

Kesi hiyo imesikilizwa leo Oktoba 06, 2025 katika Mahakama Kuu ya Tanzania (Masjala Kuu Dodoma) katika Shauri la Kikatiba Na. 24027 la mwaka 2025, ambapo Mpina anapinga kuondolewa kugombea nafasi hiyo dhidi ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Wakati leo Mahakama ikijiridhisha kuhusu utekelezaji wa amri ya kuwasilisha hoja kwa maandishi kutoka pande zote kabla ya kutangaza tarehe ya hukumu chini ya jopo la majaji watatu Jaji Frederick Manyanda, Jaji Sylvester Kainda na Jaji Abdallah Gonzi Mahakama hiyo imepanga kutoa hukumu ya shauri hilo Oktoba 10, 2025 saa 8:00 mchana. 

 

Chanzo; Eatv

Kuhusiana na mada hii: