Hatma ya Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu, inatarajiwa kujulikana leo Jumatatu, Septemba 15, 2025, wakati Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es Salaam, itatoa uamuzi wa hatimaye kuamua kama kesi ya uhaini inayomkabili mshtakiwa (Case No. 19605/2025) itafutwa, itarudishwa Kisutu au kuendelea Mahakama Kuu.
Uamuzi huu unatarajiwa kutolewa na jopo la majaji watatu (3), likiongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru, huku majaji wengine wakiwa James Karayemana na Ferdinand. Jopo hili ndilo limepitisha masuala yote ya mapingamizi yaliyowasilishwa na Lissu.
Tundu Lissu amewasilisha mapingamizi mawili. Pingamizi la kwanza, ambalo tayari limesikilizwa, linahusu mamlaka ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kusikiliza kesi yake, huku Lissu akidai kuwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haikuwa na mamlaka ya kisheria kuendesha mchakato wa awali.
Pingamizi la pili litasikilizwa baada ya Mahakama kutoa uamuzi juu ya pingamizi la kwanza; linalenga hoja yake kwamba Hati ya Mashitaka iliyotolewa Kisutu ni mbovu kisheria, haiwezi kuendelea bila marekebisho.
Katika hoja zake, Lissu ameibua hoja tano kuu:
* Mahakama ya Kisutu haikuwa na mamlaka ya kisheria kusikiliza kesi.
* Mashitaka yanayomkabili Lissu ni ya kisiasa na hayana msingi wa kisheria.
* Hukumu ya awali na machakato wake wote katika Mahakama ya ukabidhi (Kisutu) haipaswi kuendelea kuwa na nguvu ya kisheria.
* Ana haki ya msingi ya kikatiba ya usikilizaji wa haki bila masharti.
* Anaomba kesi ifutwe mara moja na kuachiliwa huru bila masharti yoyote.
Tundu Lissu alikamatwa Aprili 9, 2024, Mimba na kupelekwa Dar es Salaam. Siku iliyofuata, Aprili 10, 2024, alishitakiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. Lissu anapinga hatua hii akisema ni kinyume cha sheria, kwa sababu sheria inataka mashitaka yapelekwe kama hatua za kisheria za kukamata mtu na kesi iendelewe katika mahakama yenye mamlaka halali.
Nyaraka za mwenendo wa kesi hazikukamilika kikamilifu; nyaraka zilizotolewa zenye mapungufu ziliibua pingamizi la Lissu. Kwa mfano, alipatiwa nyaraka za Agosti 18, 2025, ambazo ni page 116 badala ya page 103 za mchakato mzima, jambo ambalo alidai linaonyesha mapungufu na makosa yanayoweza kumzuia haki na kutikisa haki za kisheria.
Lissu anaamini kuwa makosa hayo yanayohusiana na mamlaka ya Mahakama ya Kisutu yanazuia hata Mahakama Kuu kuendelea na shauri bila kuangalia pingamizi lake.
Anakabiliwa na shitaka la uhaini kinyume na kifungu cha 39(2)(d) cha Sheria ya Kanuni za Adhabu, kilichotokana na maneno aliyoyatamka yanayohusiana na mpango wa kudhibiti au kuzuia uchaguzi mkuu wa 2025. Mashitaka haya yamevutia umakini mkubwa wa umma na vyombo vya habari, huku wananchi wengi wakisubiri kwa hamu uamuzi wa Mahakama Kuu: kuachiwa huru au kuendelea kusota rumande, jambo linaloangaliwa kuwa na athari kubwa kisiasa na kisheria nchini Tanzania.
Chanzo: Bbc Swahili