Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM Dkt Hussein Ali mwinyi amewatembelea Wafanyakazi za Kitalii Mkoa wa Kaskazini Unguja ikiwemo Makundi ya Ma Beach Boys na watembeza Watalii ambapo wametoa malalamiko yao juu ya kadhia wanazokumbana nazo katika maeneo yao ya kazi katika fukwe.
Wafanyakazi za Kitalii wametoa ya moyoni mbele ya Mgombea huyo kwa yale wanayaopitia ikiwemo kupandishwa kwa kodi kiholela sehemu za vivutio na Askari utalii kuwakoesha amani ma beach boys wakiwa katika maeneo ya fukwe.
Mgombea huyo ameahidi kukomesha yale yaliotajwa ikiwemo Polisi Utalii kuchukua rushwa na kuchukua hongo vituoni pindi kunapotokea Wafanyakazi hizo za kitalii kushindwa kufahamiana vyema.
Chanzo: Millard Ayo