Katibu wa Itikadi wa Uenezi wa CCM Taifa, Kenan Kihongosi, amemtaka Waziri Mkuu Mstaafu, Joseph Sinde Warioba astaafu kwa heshima na asiwe na chuki kwa Viongozi bali awashauri kwa hekima sio kulalamika mitandaoni kila kukicha.
Akiongea na Waandishi wa Habari Jijini Dodoma leo January 17,2026, Kihongosi amesema ““Chama chetu cha mapinduzi ambacho ni Chama cha Watanzania wote huwa hakijadili Watu, sisi tunajadili hoja na mambo ya msingi, kwahiyo kwa Mzee wetu Warioba moja tunamuheshimu, pili astaafu vizuri kama Wastaafu wengine walivyostaafu vizuri”
“Tulikuwa na Waziri Mkuu Mstaafu Msuya sijui kama mliwahi kufanya nae mahojiano yoyote amemamliza muda wake ameacha wengine waendelee na kazi, hata Mzee Jakaya namnukuu aliwahi kusema yeye akiwa Rais, Mzee Mkapa alikuwa anaenda Ikulu bila kupiga hodi na anamshauri”
“Sasa unaweza ukastaajabu kwamba Mh. Warioba amekutana na Rais siku nne hazijapita yupo tena mtandoani inasikitisha kidogo lakini tunachomuomba astaafu vizuri aendelee kupumzika lakini asiwe na chuki kwa Viongozi waliopo kwasababu ana uwezo wa kushauri na kufika kwenye mamlaka husika na kuishauri kwa hekima kuliko kwenye kulalamika kila siku mtandaoni”
“Kiongozi unapolalamika kila siku mtandaoni unakuwa na maswali mengi, kuna hoja alizungumza mfano Polisi walimsimamisha wakamwambia nini, sisi tunajua Mstaafu yoyote hata Mzee JK akipita na gari ana escort hakuna Polisi wa kusimamisha huo msafara, sasa nyie mnaweza kujua alisimamishwa au vipi, tunamuomba astaafu kwa heshima na aache ulalamishi”
Chanzo; Millard Ayo