Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Salum Mwalim, ameahidi kuanzisha mji wa kibiashara wa kisasa (Tunduma City) ili kuimarisha shughuli za kiuchumi katika mpaka wa Tanzania na Zambia.
Akiwahutubia wananchi wa Tunduma, Mwalim amesema mji huo utakuwa kitovu cha biashara za kikanda, utawezesha ajira kwa vijana, na kuongeza mapato ya taifa kupitia shughuli usafirishaji na huduma za kifedha.
Aidha, ameahidi kuboresha barabara kwa kujenga barabara za juu (flyovers) katika mji wa tunduma ili kupunguza msongamano mkubwa wa malori ya mizigo, hali ambayo kwa muda mrefu imekuwa kero kwa wananchi na wafanyabiashara.
Chanzo: Clouds Media