Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Chadema Wajitenga Sakata Kupigwa Milioni 19

Chama cha Demokrasia na Maendeleo kimejiweka kando kuhusu sakata la wizi wa Sh milioni 19 zilizochangwa kwa ajli ya Mwenyekiti wa chama hicho, Tundu Lissu.

Katika taarifa yake kwa umma jana chama hicho kimeeleza kutohusika na michango hiyo na badala yake kikimtaja kaka yake na Lissu, Alute Mughwai kuhusika na uratibu wa michango hiyo.

"Tunapenda kutoa ufafanuzi kwamba, michango kwa ajili ya Mwenyekiti wa chama taifa, iliratibiwa kupitia namba ya simu ya ndugu yake Wakili Alute Mughwai Lissu, aidha utaratibu na upokeaji wa michango hii haukufanywa na sekretarieti ya chama taifa au na kiongozi yeyote wa chama" imesema sehemu ya taarifa ya CHADEMA.

Juzi Jumatano, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Justine Masejo alitoa taarifa kwa umma akieleza jeshi hilo kumshikilia mmoja wa vijana wa chama hicho kwa tuhuma za wizi wa fedha zilizochangwa kwa ajili ya kumsaidia Mwenyekiti wa chama hicho, Tundu Lissu ambaye yupo gerezani.

CHADEMA katika taarifa yake ya jana kimetaka kutohusishwa viongozi wa chama hicho kuhusiana na suala la wizi wa michango hiyo kikijinasibu kwa uadilifu, uwazi na maadili na kwamba hakitaruhusu matumizi ya jina la chama au viongozi wake kufanikisha vitendo vinavyokiuka sheria.

 

 

Chanzo; Nipashe

Kuhusiana na mada hii: