Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, John Heche leo Februari 16, 2026 akiongea na Wanahabari nje ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar Es Salaam aivaa vikali Serikali kisa mashahidi wa siri kwenye kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa chama hicho, Tundu Lissu, adai kama wameshindwa kuwapanga vizuri mashahidi, wataweza kweli kupanga uchumi wa nchi?
Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, itaendelea kesho February 17, 2026 katika Mahakama Kuu Masijala Ndogo Jijini Dar Es Salaam
Chanzo; Wsafi Media