Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Chadema Haiko Tayari kwa Maridhiano

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema hakitakuwa tayari kwa maridhiano yenye kupambaza, kuhadaa, yenye ulaghai na yenye kuliondoa Taifa kwenye ukweli, haki na kile ambacho Taifa inataka na kusisitiza kuwa kamwe CHADEMA haitowasiliti Watanzania.

Akiongea leo January 03,2026, Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, John Heche amesema “CHADEMA, Chama chenu hakitakuwa tayari kwa maridhiano yenye kupambaza, kuhadaa, yenye ulaghai na yenye kuliondoa Taifa kwenye ukweli, haki na kile ambacho Taifa inataka, kamwe hatuwasaliti Watanzania”

“Ni ubatili na dharau kubwa kwa Watanzania kuyaita maridhiano sasa katika mazingira ambapo Serikali iliamua kwa makusudi kuwapuuza Wananchi, Vyama vya siasa na Wadau wa demokrasia juu ya hitaji la nchi kuhusu mabadiliko (reforms) ya mifumo ya uchaguzi nchini, uchaguzi batili hauishii kwenye siasa pekee, huingia moja kwa moja kwenye tumbo la mwananchi na heshima ya maisha yake ya kila siku”

“Leo ninapotoa salamu hizi ni siku ya 269, tangu Mwenyekiti wetu, Tundu Lissu alipokamatwa na kuwekwa mahabusu kwa kesi ya uongo, batili na yenye uonevu wa makusudi wakidhani atapiga magoti kusujudia sanamu”

 

Chanzo; Millard Ayo

Kuhusiana na mada hii: