Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Samia “Tumejitaidi Kusimamia Utulivu wa Kisiasa, Hamjasikia Lolote Labda Ajali”

Mgombe wa Rais tiketi ya Chama cha Mapinduzi “CCM” aweka wazi uwepo wa utulivu wa kisiasa nchini “Nataka niwaambie katika kipindi cha miaka hii mitano iliyopita tumejitahidi sana kusimamia utulivu wa kisiasa, usalama na amani ndani ya nchi yetu, hamjasikia lolote na mkisikia labda ni ajali watu wamekufa”

Ameyasema hayo kwenye muendelezo wa kampeni zake wakati akizungumza na wakazi wa Chake Chake, Pemba Septemba 20,2025.

Ambapo aliendelea kwa kusema “ Mtu atakwenda kuchokoza mwenyewe na kuvunja amani ndiye atakayeshughulikiwa. Hata wale waliovuka mipaka na kutaka kuleta vurugu ndani ya nchi yetu tuliwashughulikia na hawajathubutu kurudi tena. Niwaombe sana ndugu zangu katika kipindi hiki ni kipindi wengine wanatumia kuchokozana”

“Niwaombe msichokozeke, kuweni kama mimi mama yenu, dada yenu, bibi yenu, ndugu yenu, nachokozwa sana lakini sichokozeki- kwahiyo niwaombe sana msichokozekez tusivunje amani kwasababu ya uchaguzi.”

Zaidi akaendelea kwa kusema “Akiumia mmoja imeumia familia, familia itahangaika, tusiende kuvunja amani kwasababu ya uchaguzi, sisi wote ni wamoja, kwahiyo sitafurahi kuona ndugu huku Makunduchi au Pemba kapigwa kaumizwa.”

Sisi wote niombe sana tutunze amani na utulivu na niwatoe hofu kwamba tarehe za kupiga kura hakutakuwa na vurugu yoyote, tokeni kwa wingi kapigeni kura, Vyombo vya ulinzi na usalama vimejipanga vyema kuilinda nchi hii na mimi ndiye Amiri Jeshi Mkuu ninayesema hapa, tumejipanga vyema hakutakuwa na nywinywi wala Nywinywinywi.” - Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan

Chanzo; Tanzania Journal

Kuhusiana na mada hii: