Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Bwege Apiga Chini ACT Apindukua CDM

Aliyekuwa Mbunge wa Kilwa Kusini, Selemani Said Ally Bungara maarufu kama “Bwege”, ametangaza rasmi kujiondoa katika chama cha ACT Wazalendo.

Katika taarifa yake aliyoitoa kwa umma jana Februari 18,2026 Bwege ameeleza kuwa uamuzi huo umetokana na hiyari yake mwenyewe kama mtu huru, baada ya kutafakari kwa muda mrefu na kugundua kuwa ACT Wazalendo si “rafiki sahihi” katika safari yake ya kisiasa kama alivyokuwa amefikiria awali.

Bwege, ambaye anajulikana kwa msimamo wake thabiti na lugha za mvuto majukwaani, amebainisha kuwa mwelekeo wa sasa wa ACT Wazalendo ni tofauti na matarajio yake, jambo lililompelekea kuamua kutafuta jukwaa lingine la kuendeleza mapambano ya kisiasa.

“ACT Wazalendo si rafiki sahihi kwangu, nilivyofikiria ni tofauti na nilivyohisi. Kuanzia sasa mimi si mwanachama wa ACT Wazalendo tena kuanzia tarehe 18/2/2026.Mengine nitaongea baadaye. Ninategemea kushirikiana na kulitumia jukwaa la CHADEMA katika siasa za kudai demokrasia na maendeleo la taifa langu nilipendalo-Tanzania”, ameandika Bwege.

 

 

Chanzo; Nipashe

Kuhusiana na mada hii: