Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Polepole Awajibu Polisi Baada ya Kuitwa

Baada ya Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) kumuita aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba, Humphrey Polepole kutoa maelezo na ushahidi wa tuhuma alizoibua mtandaoni, yeye amesema ipo nia njema na ovu kwenye wito huo.

Kwa mujibu wa Polepole, ipo dhamira njema na ya dhati kwenye wito wa polisi wa yeye kuhitajika kutoa maelezo na ushahidi na upande wa pili, ipo nia ovu kwenye wito huo, hivyo akahoji kwa nini wasimhoji kwa njia ya mtandao.

"Kuna watu wanataka niende pale Polisi ukifika pale unakamatwa, kwa sababu hakuna sehemu wamesema kuna tuhuma kwangu, unaweza ukaachiwa halafu baadaye unapotea na Polisi hawahusiki,” amesema Polepole jana Septemba 18, 2025 alipozungumza kwa njia ya mtandao akijibu wito wa polisi.

Polepole amesema kuitwa kwake ni dalili njema kwamba, Jeshi la Polisi limesikiliza na kuona mahali penye viashiria vya jinai, hivyo kuona vema wamtafute awaongezee maelezo na ushahidi.

"Hili ni jambo jema na huu ni upande mmoja. Unajua wananchi huko mtaani wana mashaka kweli na hii kitu inaniumiza, ni waoga mno, watu wanakutumia ujumbe mtandaoni samahani endelea kusema," amedai.

Upande wa pili, amedai ni ujanjaujanja akieleza jeshi hilo limemtafuta bila mafanikio, akihoji endapo kuna mtu ndani ya Serikali anayemtaka akamkosa kwa njia ya mawasiliano.

 

Chanzo; Mwananchi

 

Kuhusiana na mada hii: