Mtiania wa nafasi ya Urais Zanzibar kupitia Chama cha United Peoples Democratic Party (UPDP), Mohammed Ibrahim amesema iwapo atapewa ridhaa ya kuongoza visiwani hivyo, atajenga vinu vya nishati ya nyuklia.
Amesema vinu hivyo vitakuwa kwenye visiwa vya Unguja na Pemba lengo likiwa ni kuimarisha usalama pamoja na kuwa na nishati ya uhakika ya umeme.
Ibrahimu ameyasema hayo leo Septemba mosi, 2025 mjini Unguja, Zanzibar wakati akikabidhiwa fomu za kuwania kuteuliwa kuwania nafasi hiyo. Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), Jaji George Joseph Kazi ndiye aliyekabidhi fomu hizo kwa Ibrahim.
“Nikichaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar nitajenga vinu viwili vya nyukilia kimoja Unguja na kingine Pemba. Hii ni kuimarisha usalama wa Taifa, lakini vitawezesha kuwa na uzalishaji wa umeme wa uhakika ambao utatumika kwenye viwanda,” amesema
Stori inapatikana kwenye ukurasa rasmi wa Mwananchi