Naibu Katibu Mkuu, CHADEMA Bara, Amani Golugwa amesema Chama hicho mpaka kinafikisha miaka 33 kimekuwa na safari ya machozi, jasho na damu ambapo amesema katika safari hiyowamelipa garama kuwa ya mapambano ya Kidemokrasia.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa wiki ya siku ya kuzaliwa CHADEMA, Golugwa amesema "Safari ya miaka 33 ya machozi, jasho na damu, katika safari hii Chadema imepitia majaribu mazito ambayo chama kingine chochote kingeshasambaratika”
“Tumelipa gharama kubwa ya mapambano ya kidemokrasia, tumepokea mashujaa wetu, wengi waliouawa kikatili” Amani Golugwa, Naibu Katibu Mkuu CHADEMA Bara
Chanzo; Millard Ayo