Gari analotumia Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha CHAUMMA Salum Mwalim, limepigwa jiwe kwenye kioo cha nyuma na Mtu asiyejulikana muda mfupi baada ya kumshusha Mgombea huyo Hotelini Mafinga, Mkoani Iringa.
Mkuu wa msafara huo, John Mrema amesema tukio hilo limetokea usiku huu wakati Wasaidizi wa Mgombea walipotoka kutafuta chakula na huduma za dawa, ndipo mawe yaliporusha dhidi ya gari hilo na kuharibu kioo hicho ambapo OCD wa Mafinga amesema Polisi wamewakamata Watu wanne kuwahoji kutokana na tukio hilo.
Gari hili ni miongoni mwa Magari yaliyotolewa na Tume ya Uchaguzi kusaidia usafiri wa Wagombea urais katika kipindi cha kampeni.
Chanzo: Millard Ayo