Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Kihongosi, CCM Tutasimamia Serikali Sio Serikali Kusimamia Chama

Katibu wa NEC-Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi, Kenani Laban Kihongosi, leo Jumatano Novemba 19, 2025 akizungumza na waandishi wa habari amesema wajibu wa Chama Cha Mapinduzi ni kwenda kuisimamia serikali na sio serikali kwenda kukisimamia Chama.

Kenani ameyasema hayo huku akiwataka wateuliwa wote waende wakawajibike kwani Chama hakitosita kumchukulia kiongozi yeyote wa serikali, iwe mchaguliwa ama mteuliwa atakayekwenda kufanya kazi kwa maslahi yake binafsi.

Aidha, Mwenezi Kenani amewataka viongozi wote wa serikali ikiwemo wa Mikoa na Wilaya waende kufanya kazi kuhakikisha matarajio na maono ya Rais Samia Suluhu Hassan yanakwenda kukamilika, hivyo Chama hakitosita kuwachukulia hatua viongozi wavivu, wazembe na watakaoendekeza tamaa za rushwa.

 

Chanzo; Clouds Media

Kuhusiana na mada hii: