Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema mafanikio makubwa ya maendeleo yaliyopatikana katika uongozi wa awamu ya Nane yamechangiwa na kudumu kwa amani, pamoja na mipango ya muda mrefu na mfupi ambayo wamejiwekea.
Akizungumza na jopo la wahariri na waandishi wa habari Ikulu Zanzibar, Rais Dkt. Mwinyi amewatoa hofu wananchi kwamba maendeleo yaliyofikiwa na serikali yake, hayatailetea Zanzibar mzigo wa madeni na badala yake serikali itakopa na kurejesha mikopo yote huku akisistiza kuwa ataondoka madarakani akiwa amelipa madeni yote kwa sababu mipango ya fedha ipo na inaleta matokeo chanya
Pia Dkt. Mwinyi amesisitiza;
1. Ukusanyaji bora wa mapato na matumizi sahihi ya fedha za Serikali.
2. Uwezo wa Serikali kukopa na kuendesha miradi mikubwa, kutokana na nidhamu ya kifedha na utaratibu bora wa kulipa madeni.
3. Uanzishwaji wa akaunti maalum ya kulipia madeni (Debt Management Account) ambapo Serikali huweka dola milioni 15 kila mwezi (sawa na dola milioni 180 kwa mwaka).
4. Kuwekeza katika maendeleo ya wataalamu wa ndani na kuimarisha vyuo vya amali ili kuwajengea vijana stadi za kazi za kuajiriwa na kujiajiri.
Aidha Rais Dkt. Mwinyi amewasihi viongozi wa dini, wanasiasa na waandishi wa habari kuendelea kuhubiri amani na mshikamano kabla, wakati na baada ya uchaguzi mkuu ujao.
Stori hii inapatikana kwenye ukurasa wa instagram wa Cloudstv .