Mahakam kuu nchini Zambia imewahukumu watu wawili miaka miwili jela kwa tuhuma za kutumia uchawi kujaribu kumua Rais wa nchi hiyo Hakainde Hichilema.
Watu hao Leonard Phiri na Jasten Mabulesse Candunde walikamatwa Disemba, wakiwa na hirizi pamoja na kinyonga hai hivyo kutiwa hatiani.
Fine Mayambu, Hakimu wa Mahakama anasema “Watuhumiwa walikubali umiliki wa hirizi hizo, Phiri alionyesha kwamba mkoa wa kinyonga ambao unechomwa kutumiwa katika tambiko, ulitegemewa ungesababisha kutokea kwa kifo cha Rais.”
Hivyo hukumu hiyo ni kwaa ajili ya kukomesha vitendo hivyo kutojirudia ndani ya zambia.
Lakini kwa upande wa wakili wa watuhumiwa Aggripa Malando anasema wateja wake waliomba kuhurumiwa kwani ndio mara yao ya kwanza kutenda tukio hilo na kukiri kuwa wateja wake walitenda kosa hilo licha ya kufanya kama sehemu ya majukumu yao ya kila siku.
Zambia sio nchi pekee yenye vifungu vya sheria vinavyobainisha uchawi kama kosa linaloweza kumtia mtu kifungoni, nchi kama Afrika ya Kusini, Benin, Cameroon ni baadhi ya nchi zenye sheria hiyo.
Chanzo: Tanzania Journal