Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Sheikh Ponda Akumbushia ya Mtwara

Mgombea ubunge wa Temeke kupitia Chama cha ACT- Wazalendo, Sheikh Ponda Issa Ponda, amewa-omba wakazi wa Temeke kumchagua kuwa mbunge wao ili kuweza kuwakilisha kero zao bungeni, ka-ma alivyowahi kufanya kwa wananchi wa Mtwara wakati wa mgogoro wa gesi na mambo yakawa sawa.

Sheikh Ponda amesema hayo leo Jumatatu Septemba 15 2025, alipokuwa akizindua kampeni za ub-unge za chama hicho zilizofanyika Kata ya Tandika Devis kona relini jijini Dar es Salaam.

Katika kuwaomba huko kura, Sheikh Ponda amesema hataki ubunge ili kuwa maarufu au kupata fedha kwa kuwa, kazi za kuwatetea wananchi amezianza siku nyingi na kukumbushia alipowatetea wananchi wa Mtwara kipindi cha mgogoro wa gesi yao, huku wakiwa hawajui watakavyofaidika na hatua hiyo.

"Ukiangalia mimi sio mtu wa Mtwara ni wa Kigoma lakini niliwapambania watu wa huko hadi kuona haki inatendeka.

"Hivyo, nitakapopata ridhaa naamini nitakuwa mwakilishi mzuri wa kwenda kuwakilisha yale ambayo yametokana na wananchi wa Temeke," amesema Sheikh Ponda.

Mgombea huyo amesema kwenda bungeni haendi kutafuta umaarufu wala fedha, bali ni kupata nafasi ya kuweza kukaa katika vikao vya mamlaka ili kuwatetea wananchi.

 

Chanzo; Mwananchi

Kuhusiana na mada hii: