Binti wa Rais wa Cameroon Brenda Biya (27), ameushangaza umma baada ya kutoka hadharani na kuwaomba Wananchi wa Cameroon wasimpigie kura Baba yake Paul Biya, katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 2025.
Brenda ameutumia mtandao wake wa Tik Tok kuutangazia umma wa Wacameroon ambapo
alimlaumu Baba yake kwa ya hali umasikini, ukosefu wa ajira na kudumaa kwa maendeleo nchini humo, tukio hilo likiwa la kwanza kuwahi kutokea barani Afrika kwa Mtoto wa Rais aliye madarakani kumpinga mzazi wake kisiasa hadharani bila wasiwasi.
Rais Paul Biya (92), amekuwa madarakani tangu mwaka 1982 na kwa mwaka huu anagombea Urais kwa awamu ya saba mfululizo, hata hivyo Brenda ambaye kwa sasa anaishi nchini Uswizi ameonesha waziwazi kutokuwa na mahusiano mazuri na familia yake akiwashutumu kumtenda vibaya kitendo kilichozua maswali ikiwa mtizamo wake unaakisi hali halisi nchini Cameroon.
Chanzo; Millard Ayo