Mgombea wa Ubunge Jimbo la Rufiji na aliyewahi kuwa Waziri wa Ofisi ya Rais Tamisemi, Mohammed Mchengerwa, amehudhuria kampeni za Ubunge Jimbo la Makunduchi na kunadi sera huku akimuombea kura Mgombea Ubunge wa Jimbo hilo, Wanu Hafidhi Ameir, akimwelezea kama Mwalimu wake wa siasa.
Mchengerwa amesema changamoto zinazowakabili Wananchi wa Makunduchi zitapatiwa majibu chini ya uongozi wa Wanu, huku akiwaombea kura pia Mgombea Urais wa Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi na Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Mkutano huo umefanyika katika Viwanja vya Muyuni, Jimbo la Makunduchi, Kusini Unguja.
Chanzo; Millard Ayo