Serikali ya kijeshi ya Burkina Faso imetangaza kuondoa ada zote za VISA kwa Raia wote kutoka Mataifa ya Afrika ikiwa ni hatua ya kuimarisha harakati za ujumuishaji wa Bara la Afrika na kurahisisha usafiri wa Watu na bidhaa.
Waziri wa Usalama wa Ndani wa Taifa hilo Mahamadou Sana baada ya Kikao cha Baraza la Mawaziri kilichoongozwa na Kiongozi wa Kijeshi Capt Ibrahim Traoré amenukuliwa akieleza yafuatayo “kuanzia sasa Raia yeyote wa Nchi yoyote ya Afrika anayetaka kuingia Burkina Faso hatolipa chochote kwa ajili ya VISA”
Aidha, hatua hii inaifanya Burkina Faso kuungana na Nchi kama Ghana, Rwanda na Kenya ambazo tayari zimeshachukua hatua za kupunguza masharti ya usafiri kwa Wageni kutoka Bara la Afrika.
Capt Ibrahim Traoré ( 37), Mwanajeshi Kijana aliyechukua madaraka kwa mapinduzi ya kijeshi mwaka 2022, amejizolea sifa nyingi toka alipoanza kuliongoza Taifa hilo kijeshi mwaka 2022.
Chanzo: Millard Ayo