Mgombea Ubunge Arusha, Poul Makonda amelezea kuwa haitakubalika katiba ivunjwe kwa maneno ya mtandaoni huku akisisitiza kuwa hatuna nchi nyingine isipokuwa Tanzania.
Aneyasema hayo l Katika Muendelezo wa Kampeni Chama cha Mapinduzi CCM, huko Wilayani Sengerema, Mwanza Oktoba 7,2025
“Tanzania hii imejengwa kwenye misingi imara chini ya Waasisi wetu na mwendelezo wake umefanywa na Rais Samia hatuna udini wala ukabila, niwaombe sana hatuna nchi nyingine zaidi ya Tanzania”
Akigusia kifo cha akiyekuwa Rais wa awamu ya tano Hayati John Pombe Magufuli, amesema “Uchaguzi huu ni wa kikatiba, sio matakwa ya Mtu wala hisia za Mtu na nchi haiendeshwi kwa matamko tunaendesha kwa mujibu wa Katiba, Dkt. Samia alipoondoka Duniani Dkt. Magufuli aliapa kuilinda Katiba na sisi Wana CCM hatutokubali aivunje Katiba kwa kuruhusu kelele za kwenye mitandao”
“Na wengi wanaofanya uchochezi ukiwatazama wana passport na wengine hawapo nchini wapo kwenye nchi zao kule, niombe sisi tulioko hapa, tulioona kazi inayofanywa na Dkt. Samia tuendelee kumuunga mkono, tusikubali, tusikubali, tusikubali kutumika” - Poul Makonda
Chanzo: Tanzania Journal