Viongozi wa Jamii ya Kimasai (Malaigwanan) pamoja na Viongozi wa Vijana upande wa jamii ya Kimila ya Wamasai waliopo Monduli Mkoani Arusha wameiomba Serikali kufika katika kijiji hicho na kulichunguza Kanisa la Pentekoste juu ya mahubiri yake ambayo wamedai yamekuwa yakiingilia shughuli za kimila, Kuvunja ndoa za watu pamoja na kuzuia watu wa jamii kufanya shughuli za kimila.
Hayo yameelezwa na viongozi hao wa kijiji kupitia mkutano uliofanyika katika kata ya Lepurko hii ni kufuatia kuwepo madai kutoka kwa viongozi wanne wa Makanisa hayo waliodai kuvamiwa na vijana wa jamii ya Kimasai na kutembezwa uchi porini ambapo viongozi wa kimasai wamesema kuwa hawataki vurugu bali wameiomba Serikali kufika ili kuweza na kufanya mazungumzo na pande zote ili kufikia muafaka.
“Mimi Laigwanani mlezi wa vijana ambao ni Nyangulo kwa jina maarufu mpenda amani, hawa watu wa Kanisa hawa hatujui tumewakosea nini mpaka tunakamatwa na tunaheshimu kila mtu, kwa hiyo sisi mila yetu hatuwezi kuiacha ila kama sisi tumewavamia watu vibaya tuulizwe kwa sababu sisi Malaigwanani ni wasuluhishi na watu ni watu wakutokomeza ubaya” amesema Mlezi wa Vijana jamii ya Kimasai.
Chanzo; Millard Ayo