Wakili Peter Kibatala kwa niaba ya Mawakili wa Humphrey Polepole ambaye amehudumia Tanzania katika nyadhifa mbalimbali za utumishi wa umma, wamezitaka Mamlaka za Usalama wa Raia na Mali zao Nchini Tanzania kutumia mbinu na rasilimali zote za umma kuhakikisha na kutoa taarifa kwa Umma wa Watanzania na Dunia kwa ujumla kuhusu hali ya usalama na maslahi ya kisheria ya Humphrey Polepole.
Taarifa iliyosambazwa na Wakili Kibatala leo October 06,2025, imenukuliwa ikieleza yafuatayo “Tutaendelea kutoa taarifa zaidi juu ya suala hili, zikiwemo hatua tunazozichukua kwa kushirikiana na Watu na Taasisi mbalimbali Duniani kote”
Chanzo: Millard Ayo