Waziri wa Afya Mhe. Mohamed Mchengerwa amezitaka hospitali za Rufaa nchini kuhaikikisha zinafanikisha utaratibu wa kupata ithibati za kimataifa ili kutambulika kwa urahisi na kuvutia tiba utalii nchini
Akizungumza Januari 05, 2026 Jijini Dar es Salaam alipokuwa taasisi ya saratani ya ocean road (ORCI) kwa ziara na uzinduzi wa bodi ya wadhamini ORCI, Waziri Mchengerewa amemuelekeza katibu Mkuu kuhakikisha hospitali zote za rufaa zipate Ithibati za kimataifa ili kuvutia tiba utalii sababu vifaa tiba vipo vya kutosha tayari
“Serikali ya awamu ya sita imefanya kila linalowezakana kuhakikisha hospitali zote zinakuwa na vifaa tiba vya kutosha na kupeleka huduma kwa wananchi, natoa maelekezo Katiby Mkuu hakikisha hiz hospitali zinapata Ithibati za kimataifa ili kuvutia tiba utalii kutoka kwa mataifa mbalimbali” amesema Waziri Mchengerwa
Amesema kupata ithibati ya kimataifa ni hitaji la msingi la kuhakikisha ubora wa huduma, usalama wa mgonjwa na ufanisi wa mifumo ya taasisi, huku akiitaka taasisi ya saratani ya ORCI kuwa mbele kwenye mchakato wa kupata ithibati ya kimataifa
“Nisitize kwamba kupata ithibati ya kimataifa si anasa bali ni hitaji la msingi kwetu sote kwenye kuhakikisha kwamba tunakuwa na ubora wa huduma, usalama wa mgonjwa na ufanisi wa hali ya juu wa mifumo yetu ya taasisi” – ameeleza Waziri Mchengerwa
Aidha Waziri Mchengerwa ameupongeza uongozi wa taasisi ya saratani Ocean Road kwa kuanza mchakato wa kupata ithibati hiyo ambayo inatarajiwa kupatikana baada ya miaka itakuwa imeshakamilika
Chanzo; Bongo 5