Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Askari Aliyemuua Mwenzaka Ajiua Njombe

Askari wa Jeshi la Magereza mkoani Njombe Erasto Mlelwa (26) amejiua kwa kujirusha kutoka kwenye gari la polisi baada ya kubainika kushiriki mauaji ya askari mwenzake wa jeshi hilo Dickraka Mwamakula (24) huko Lilondo halmashauri ya Madaba mkoani Ruvuma.

Hayo yamebainishwa Septemba 21,2025 na kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Mahamoud Banga wakati akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya jeshi la polisi mkoani humo.

Amesema jeshi hilo lilikuwa linaendelea na uchunguzi kufuatia taarifa za kupotea kwa askari Dickraka Mwamakula ambaye alilipotiwa kupotea tangu Septemba 7,2025 ambapo mara ya mwisho alikuwa na askari mwenzake Erasto Mlelwa.

Amesema askari hawa walielekea eneo moja lililofahamika kwa jina la Lilondo huko Madaba kwa ajili ya kuangalia Mashamba lakini baada ya hapo Mwamakula hakuweza kuonekana mpaka jeshi la polisi lilipoanzisha uchunguzi wa kina.

Ambapo watuhumiwa hao wote wawili baada ya mahojiano waliweza kuonyesha mwili wa Dickraka mahali ulipo ukiwa na majeraha makubwa eneo la kisogoni lakini mwili wake ukiwa umechomwa moto na kufukiwa katika eneo la mashamba.

Wakati jeshi la polisi linaenda hospitali ya Lilondo kwa ajili ya kumpata daktari ili kufanya uchunguzi wa mwili huo (postmortem) mtuhumiwa Erasto Mlelwa aliamua kujiondoa uhai wake kwa kuruka kutoka kwenye gari na kuangukia kichwa.

Mwili wa marehemu Dickraka umehifadhiwa katika hospitali ya Kibena kwa ajili ya taratibu zingine za mazishi lakini mwili wa Erasto Mlelwa ambaye amejiua upo huko Madaba kwa ajili ya kusubiri uchunguzi wa daktari. 

 

Chanzo: Eatv

Kuhusiana na mada hii: