Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu amegoma kuendelea na kesi ya uhaini inayomkabili Mahakama Kuu ya Tanzania Masijala Ndogo ya Dar es Salaam kutokana na baadhi ya Wafuasi wa Chama hicho kutokuwepo mahakamani.
Lissu alifikishwa mahakamani hapo mapema asubuhi ya leo kwa ajili ya kuendelea na kesi yake mbele ya Jopo la Majaji watatu akiwemo Jaji Dunstan Ndunguru lakini baada ya kutokuwaona baadhi ya Wanachama wa Chama hicho aliibua hoja ya kugoma.
Lissu alidai amepata taarifa baadhi ya Wafuasi wa CHADEMA wamegoma kutokana na wenzao kuzuiliwa kuingia mahakamani na Maafisa wa Jesho la Polisi hivyo hawezi kuendelea na kesi hadi suala hilo litolewe muongozo na Mahakama.
Hata hivyo Wakili wa Serikali Mkuu Nassor Katuga aliiomba Mahakama kuendelea na ratiba zake kwa maana suala analoliwasilisha Lissu halina uhalisia na Majaji wameahirisha kwa muda kesi hiyo.
Chanzo; Millard Ayo